January 20, 2021

 


UONGOZI wa Yanga umewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia kuwa mkataba wa mshambuliaji wao mpya, Fiston Abdoul Razak una kipengele cha kuongeza mwingine baada ya huo alionao kumalizika.

Hii inatokana na ukweli kwamba kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), mchezaji anapokuwa na mkataba wa miezi sita anakuwa huru kufanya mazungumzo na klabu nyingine itakayomuhitaji.

Akizungumzia mkataba huo Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa amesema: "Niwaondoe hofu mashabiki wa Yanga kwa kuwaambia kuwa Fiston ni mali yetu na hakitatokea kitu chochote kibaya, licha ya kusaini mkataba wa miezi sita kwani yapo makubaliano mazuri kutoka pande zote mbili,"

Nyota huyo anatarajiwa kutua nchinio siku ya Ijumaa ili kukamilisha taratibu za kusaini mkataba huo.

11 COMMENTS:

  1. viongozi muwe seriousy matatizo yaanza kwenye mkataba na muelewe fistoni ni mchezaji anataka maslah sasa mkibezi kwenye mapenzi fiston hana mapenz na klabu ila ni mwajiliwa kikubwa maslah kuweni makini viongozi mnatuyumbisha

    ReplyDelete
  2. Hahahaaaa mnajidanganya, kama amesaini miez 6 basi ikiisha yuko huru pia kabla ya hapo anawezafanya mazungumzo na timu nyingine

    ReplyDelete
  3. Kwa hiyo utopolo akili zao ndo zimeishia hapo

    ReplyDelete
  4. Wanamuogopa Mnyama asije kuwapiga pute.

    ReplyDelete
  5. Tusiishi kwa mazoea, Sio kila mchezaji anaakili za Morison...

    ReplyDelete
  6. Nilisema huko awali kuwa ya morisson yanaweza kujirudia, mchezaho anasrma miezi sita, uongozi unasema miska miwili kuna mti akaporomosha matusi sana. Sasa yako wapi?

    ReplyDelete
  7. Ni Jambo la kawaida ktk mkataba maana hiyo ni win win situation hauwezi kujua performance akiwa Yanga itakuaje

    ReplyDelete
  8. Hivi mchezaji mwenye CV kubwa kiasi hicho (kwa wananvyosema) anapewa mkataba wa miezi sita. Kweli timu zetu haziko serious. Eti wanamjaribu kwanza. Mbona Samata alipewa mkataaba wa miaka 4 na Aston Villa, tena kwenye dirisha dogo. Vilabu vyetu wananshindwa nini? Halafu akichukuliwa na Simba mnaanza kupata uharo mwembamba na malalamiko kibao. Mpeni mkataba wa muda mrefu ili watakaotaka kumnunua wailipe klabu fedha ya kuvunja mkataba.

    ReplyDelete
  9. Mkataba mrefu unahitaje pesa ndefu. Wataweza wap na pesa ya kuungaunga

    ReplyDelete
  10. utopolo hoeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeew

    ReplyDelete
  11. Utopolo hiyo kawaida yao ni Kama hawashuriani poleeeeeeeeni saaaaana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic