January 28, 2021


 WALLACE Karia, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) amefanikiwa kuteuliwa kugombea nafasi ya Mjumbe wa Baraza la Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Nafasi ambayo amefanikiwa kuteuliwa Karia ni kwa nchi za Afrika zinazozungumza Lugha ya Kingereza.

Jina lake limepitishwa kugombea nafasi hiyo baada ya kufuzu kwenye kigezo cha uhakiki wa uadilifu, ukaguzi ambao hufanywa na Kamati Maalumu ya FIFA kwa wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya Shirikisho hilo.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF, uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwezi Machi 2021 nchini Morocco na Tanzania itawakilishwa na Karia. 

1 COMMENTS:

  1. NAONA ANATAFUTA PERSONAL ACHIEVEMENT WAKATI TAIFA LAKE KISOKA BADO LINACHECHEMEA, APIGWE CHINI TU

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic