January 24, 2021


 IMEELEZWA kuwa baada ya mabosi wa Simba kushindwana na Florent Ibenge ambaye ni Kocha Mkuu wa AS Vita pamoja na timu ya Taifa ya Congo kwenye upande wa maslahi sasa wameelekeza nguvu kwa Didier Gomes Da Rosa.

Ibenge alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba kuja kuchukua mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye alibwaga manyanga Januari 7.

Didier anatajwa kujiunga na Simba akitokea katika Klabu ya EL Marreikh ya nchini Sudan ambapo inasemekana kuwa amevunja mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.


Hizi hapa timu alizowahi kuzifundisha, 2008–2010 AS Roquebrune Cap Martin, 2010–2010 ES Fos sur Mer
2010–2011 Cagnes-le-Cros, 2012–2013 AS Cannes B
2013–2014 Rayon Sports, 2014–2015 Coton Sport, 2015–2016 CS Constantine, 2016–2017 JSM Skikda, 2017–2018 Ethiopian Coffee, 2019 Horoya AC, 2019–2020 Ismaily na 2020- Al-Merrikh.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameweka wazi kuwa mrithi wa Kocha Mkuu, Sven Vandebroeck atatambulishwa mapema kabla ya mashindano ya Simba Super Cup ambayo yanatarajiwa kuanza Januari 27.

"Niwaambie tu kwamba mashabiki wa Simba, kila kitu kipo sawa na mwalimu yupo ambaye ataanza kazi kabla ya mashindano ya Simba Super Cup.

"Mwalimu ana uzoefu na mechi za kimataifa na uzoefu pia wa soka la Afrika hivyo ni suala la muda tu kila kitu kitakuwa wazi," .

6 COMMENTS:

  1. Unaona uwongo unavojionesha huws. Kila siku mkisema "habari za hakika tulizoziipata Ibenge, halafu kwa lugha hiyo hiyo, Mswidin aliecheza michezo 20 bila ya kutia goli na jana ni Mfaransa nae keshafika

    ReplyDelete
  2. Msimsubiri simba wenyewe wakutangazieni kocha wao kuliko kubuni taarifa za uongo.

    ReplyDelete
  3. Mtapata tabu sn na simba hii. Simba ina viongozi wenye akili sn, c rahc kujua kinachoendelea msimbazi hd wenyew waseme. Ht huyu mliemuandika leo n kwakuwa kavunja mkataba huko el merrikh ndo mkaoanisha na kuja simba,lakn kocha mwenyew cyo huyo wala. Subirini mtapata chakuandika akishatangazwa

    ReplyDelete
  4. Mmejigeuza wapiga ramli kwani lazima muwe wankwanza kumtangaxa kocha wa Simba au sada hivi umekuwa Babra kiasi cha kujua Simba na Ibenge walishindwana kimaslahi au source yako ya habari ni mwinyi zahera

    ReplyDelete
  5. Pumbavu sana wandishi wa blog hii

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic