January 24, 2021


 PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa wapo kwenye wakati mgumu kutokana na kumkosa nyota wao Sergio Arguero ambaye anasumbuliwa na majeraha.

Arguero ambaye ametumika ndani ya City kwa muda wa miaka tisa na nusu mkataba wake unakaribia kumeguka na anatajwa kutoongeza mkataba mwingine.

Amekuwa mhimili ndani ya City akiwa amecheza jumla ye mechi 379 na kutupia jumla ya mabao 256 anasumbuliwa na goti ambalo aliumia msimu uliopita.

Jitihada za kurejea kwenye ubora zimekuwa zikikwama kwa kuwa amecheza mechi tano pekee ndani ya City msimu huu.

Guardiola amesema kuwa anatamani kumuona Aguero akiwa uwanjani ila hana namna ya kufanya.

"Tumemkumbuka kwa anachokifanya na hakuna namna ambayo tunaweza kuifanya kwa sasa. Uwezo wake unaonekana na ni moja ya washambuliaji wazuri," .

1 COMMENTS:

  1. Ana hernia isije ikawa na yeye Man United wamemloga!
    Waandishi wa Tanzania kywenu serious.Nyie ni kioo cha kutoa habari wacheni ushamba na upumbavu wa karne ta ujima.Eti kulogana mnakupa publicity ya maana. Tunaonekana wajinga kuamini mambo ya kipumbavu. Mtu anaishi kwenye nyumba ya tembe atawezaje kukupa wewe utajiri?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic