AKIWA sehemu ya wachezaji walioanza rasmi mazoezi kwenye siku ya kwanza ya kocha mpya wa Simba Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa kiungo mshambuliaji wa Simba raia wa Zambia, Larry Bwalya alionyesha uwezo mkubwa kiasi cha kupokea pongezi nyingi kutoka kwa Mfaransa huyo.
Mazoezi hayo yanaendelea kufanyika katika viwanja vya Simba Mo Arena vilivyopo Bunju ambapo kikosi hicho kinajiandaa na michuano maalum ya Simba Super Cup itakayoanza kutimua vumbi kesho Jumatano.
Mzambia huyo alionyesha ufundi mkubwa katika umiliki wa mpira, kupiga pasi za maana pamoja na kukaba kiasi cha kocha mkuu kusikika akimpongeza mara kwa mara.
Akizungumzia kuhusu viwango vya wachezaji wake baada ya kusimamia mazoezi hayo Da Rosa alisema: “Bado ni mapema sana kuzungumzia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja kwa sasa kwa kuwa sijawaona wachezaji wote, lakini nimefurahishwa na namna ambavyo mazoezi yamefanyika Simba ni klabu kubwa na ina wachezaji wengi wazuri ambao wanazidi kunipa moyo wa kufanya vizuri,"
Pambana kijana
ReplyDeleteA shiny day begins in the morning
ReplyDelete