January 21, 2021

 


KIUNGO mkabaji wa klabu ya Simba, Jonas Mkude amejitokeza rasmi na kuomba radhi kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu zilizokuwa zikimkabili.

Mkude ambaye ni mchezaji Mwandamizi wa kikosi cha Simba hajaichezea Simba tangu  Desemba 23, mwaka jana alipocheza mchezo wa michuano ya klabu bingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.

Akiomba radhi hiyo Mkude amesema: "Tumeumbwa kukosea lakini haimaanishi nitakosea tena, mimi ni Mwanasimba mwenzenu na klabu hii ni sehemu ya maisha yangu.

"Naamini wachezaji wenzangu, benchi la ufundi, viongozi, wanachama na mashabiki mtanielewa na kunisamehe,"


6 COMMENTS:

  1. Njaa haina baunsa!!!

    ReplyDelete
  2. Wee uliekoment hapo juu kuwa mkude ana njaa una uasili ya ushetani ndani ya nafasi yako. Sema tu kuwa imekuuma kuona Mkude anarejea simba.Alichokifanya Mkude ni kitu kikubwa na cha kupongezwa na kutiwa moyo na kujengwa zaidi kisaikolojia. Kuna watu wanatamani kuona mkude akipotea kabisa.Kila mtu ana udhaifu wake na ndio maisha. Kuna wale wanaotambua madhaifu yao na kujirekebesha na kuna wale amabao wana madhaifu na kuyachukulia kama ni aina ya maisha yao ambayao wameamua kutaishi nayo.Mkude ana uwezo wa kucheza mpira nje na ndani ya Tanzania kwenye malachi mazuri,si mtu wa kulia njaa. Na kujishusha sio udhaifu bali ni uadilifu katika maisha.Tuwapongeze tu simba kwa kusimamia nidhamu maana kuna watu kadhaa waliamua kwa makusudi kupotosha msimamo wa simba juu ya Mkude kwenye kusimamia nidhamu yake.Mkude kakulia simba wana uchungu nae kuliko hao wanaoropokwa hovyo.Kama simba wangekuwa na ubaya na mkude asingedumu ndani ya simba zaidi miaka kumi 10.

    ReplyDelete
    Replies
    1. We dada unaonekana ni kahaba sugu kwa jinsi ulivyotoa povu lote hilo hadi kufikia hatua ya kumwambia mwenzio ana asili ya ushetani.Ulipaswa ujiulize ni mara ngapi huyo basha wako amekuwa anafanya vitendo vya utovu wa nidhamu na kuonywa lakini amekuwa anaonesha kiburi na hata aliposimamishwa aliendelea kutoa maneno ya dharau kwa uongozi lakini bado unaleta utopolo wako hapa.Kwa hakika mimi ni mmojawapo wa wasiotaka arudi kundini baki naye huko huko uhangaike naye sisi tunajipanga kwa mapambano yaliyo mbele yetu

      Delete
  3. Sawa ulivofanya Mkude. Kweli makosa ni kitu cha kawaida. Penseli mbele kuna risasi ya kuandikia na nyuma kuna raba ya kufuta makosa na anayekiri makosa yake ina mana hatoyarejea, lakini yeye haikuwa hivo na amekuwa akiyarejea tena na tena na Mkude ajue umri wa utundu umeshamuacha mkono. Umri ni kama maji ya mto ambapo maji yapitayo huwezi kuyagusa mara mbili kwasababu yaliyopita hayatorudi tena na umri ndivo ulivo. Mpira ndio maisha yake na Simba imekuwa kama ni baba na akenda kokote utaonekana kama mtoto wa kambo mwenye kukosa pendo la hakika Alilolipata ni somo tosha, ajitulize kwani majuto mjukuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakubaliana na maoni yako mdau maana kwa umri alionao Mkude na muda aliokaa Simba ingetosha kabisa awe mfano mwema lakini ndo hivyo tena!

      Delete
  4. Big time mkude ulitukera mashabiki wako ila karibu japo hasara ni kubwa sana tumeipata hata timu yetu ya Taifa pengo lako linaonekana sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic