OLE Gunner Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa wamegadhabika kwa matokeo ambayo wamepata usiku wa kuamkia leo kwa kunyooshwa mabao 2-1 dhidi ya Sheffield United.
Wakiwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, walishuhudia pointi tatu zikisepa mazima na kubaki na pointi zao zilezile 41 baada ya kucheza jumla ya mechi 20.
Bao la Harry Maguire dakika ya 64 akisawazisha bao la Keane Bryan lililopachikwa dakika ya 23 halikufua dafu kwani waliokota bao la pili dakika ya 74 lililofungwa na Oliver Burke na kuifanya United kuwa nafasi ya pili huku kinara akiwa ni Manchester City mwenye pointi 41.
Sheffield United ambao hali yao ni mbaya ndani ya Ligi Kuu England wakiwa nafasi ya 20 wanaongeza pointi tatu na kufikisha jumla ya pointi 8 na kusalia hapohapo baada ya kucheza jumla ya mechi 20.
Ole amesema:"Kiukweli tumegadhabika tulikuwa tunahitaji pointi tatu ila tumekosa, kwa kilichotokea hamna namna tutajipanga mechi zijazo.

"Wachezaji wamepambana kwa kadri ya uwezo wao ila hawakuwa na namna wamecheza vizuri ila wameshindwa kufunga," .
0 COMMENTS:
Post a Comment