January 28, 2021


 PETER Mudhuwa, beki mpya ndani ya Klabu ya Simba, raia wa Zimbabwe amesema kuwa anataka kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza kutakachoanza kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Beki huyo amesaini dili la miezi sita anakutana na ukuta wa Simba unaoongozwa na Joash Onyango,Ibrahim Ame, Pascal Wawa na Kennedy Juma kwa upande wa mabeki wa kati.

Anakuwa chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes ambaye jana, Januari 27 kwa mara ya kwanza alishuhudia wachezaji wake wakicheza mchezo wa ushindani mbele ya Al Hilal na kusepa na ushindi wa mabao 4-1.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa nyota huyo hakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza wala wale ambao walikuwa kwenye benchi.

Nyota huyo amesema:"Ninajua kwamba Simba nì timu kubwa na ina mabeki wenye uwezo ila nitapambana ili kupata namba kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Haitakuwa kazi rahisi ila inawezekana kwa kupambana na kuongeza juhudi kwenye mazoezi nina amini nitapata namba na kazi yangu nitaifanya kwa umakini," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic