PRINCE Dube, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ameanza makeke yake baada ya kufunga bao wakati timu yake ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Zanzibar Combine.
Azam FC imeweka kambi Visiwani Zanzibar ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho ambapo ikiwa huko mpaka sasa imecheza jumla ya mechi tatu za kirafiki.
Mchezo wa Kwanza ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Mlandege ambapo nyota huyo alitoa pasi moja ya bao na mchezo wa pili walipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya KMKM na mchezo wa tatu walishinda mabao 2-1 dhidi ya Zanzibar Combine.
Ikiwa imefunga jumla ya mabao manne na kufungwa matatu amehusika Kwenye mabao mawili, amefunga moja na pasi moja ya bao.
Ndani ya Ligi Kuu Bara amefunga mabao sita na kutoa pasi nne za mabao akiwa ni kinara ndani ya Klabu ya Azam FC.
Dube amesema:"Nilikuwa nje kwa muda mrefu sasa ni wakati wa kuendelea kupambana kwa ajili ya timu na kufanya vizuri bado kuna nafasi ya kufanya vizuri," .
Alikuwa nje kwa muda wa wiki sita baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambapo Azam ilipoteza kwa kufungwa bao moja kwa bonge.
0 COMMENTS:
Post a Comment