MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania, Ditram Nchimbi amesema kuwa jitihada zinahitajika kwa ajili ya timu ya Taifa ya Tanzania hivyo watapambana bila kuchoka kwa ajili ya Tanzania.
Kwa sasa Stars ipo nchini Cameroon kwa ajili ya kushiriki michuano ya Chan ambayo inawahusu wachezaji wa ndani.
Ikiwa kundi D, imecheza mchezo mmoja dhidi ya Zambia Januari 19 na kuambulia kipigo cha mabao 2-0 kwenye mchezo wa ufunguzi.
Ina kazi nyingine Jumamosi, Januari 23 kusaka ushindi mbele ya Namibia ambapo ikimaliza dakika 90 kwa wapinzani hao itakuwa na mchezo mmoja mkononi.
Nchimbi amesema kuwa bado wana kazi ya kupambana kwa ajili ya Taifa la Tanzania ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.
"Bado tuna kazi ya kufanya zaidi ili kufikia malengo kwani ushindi wetu ni ushindi wa Watanzania wote hivyo jitihada zinahitajika," .
0 COMMENTS:
Post a Comment