KIUNGO mshambuliaji hatari wa klabu ya Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’
ameweka bayana kwamba ndoto zake ni kuhakikisha anajenga historia katika kikosi
hicho kwa kufanya vizuri kwa muda ambao atakuwepo.
Nyota huyo ameongeza kuwa atakachofanya ni kuipambania timu
hiyo kwenye kila mechi ambayo atacheza kwa ajili ya mwisho kutwaa mataji.
Saido ambaye tayari amefanikiwa kutwaa kombe moja akiwa na kikosi cha Yanga baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa taji la Kombe la Mapinduzi baada ya kuwafunga
Simba Januari 13, mwaka huu.
Mzaliwa huyo wa Burundi amesema: “Nimejipanga kuhakikisha mzunguko wa pili nacheza kwa kiwango bora zaidi kuliko ilivyo kwa sasa, kwani nataka kuhakikisha timu inafanya vizuri na kufanikisha kila ambacho tumekipanga,”
Kila la kheri sheikh
ReplyDeleteAsante Bwana Saido
ReplyDelete