January 19, 2021

 


MENEJA wa mshambuliaji Reliants Lusajo, Ahmad Kassim ‘Prezdaa’ amesema kuwa sababu kubwa za mteja wake kuipiga chini KMC baada ya kukipiga kwa miezi sita tu na kurejea tena Namungo ni nyota huyo kukosa furaha akiwa na kikosi hicho cha Wanakinondoni.

Lusajo aliyetajwa kuhitajika na Yanga kwenye dirisha la usajili la mwezi Agosti, alijiunga na KMC mwanzoni mwa msimu huu, na kusaini kandarasi ya mwaka mmoja ambayo ameitumikia kwa miezi mitano pekee baada ya kufikia makubaliano maalum ya kuvunja mkataba huo.

Akiwa na KMC msimu huu Lusajo ameifungia klabu hiyo mabao 4 ambapo alikuwa akiongoza chati ya wafungaji ndani ya kikosi hicho.

Nyota huyo msimu uliopita aliifungia Namungo mabao 12 hivyo kumaliza akiwa kinara wa ufungaji ndani ya kikosi hicho huku pia akikamatia nafasi ya nne kwenye chati ya wafungaji.

Akizungumzia kuhusu mkataba huo Prezdaa amesema: “Ni kweli tumefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na KMC kufuatia mteja wangu kukosa furaha katika kipindi cha miezi mitano aliyokuwa na KMC.

“Na kwa kuwa mikononi mwetu tulikuwa na ofa kutoka Namungo, eneo ambalo Lusajo alikulia basi tukaona ni bora turejee nyumbani kujipanga zaidi,”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic