January 15, 2021


 SAIDO Ntibanzokiza,  kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa wachezaji wenzake walimuomba awasaidie kuimaliza Simba, Januari 13 licha ya kuwa alikuwa na maumivu jambo ambalo alilifanya kwa kufunga penalti ya ushindi.

Ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Ntibanzokiza ambaye ni ingizo jipya ndani ya Yanga kwenye usajili wa idirisha dogo akiwa ni mchezaji huru kwenye Kombe la Mapinduzi kwa kuwa kwenye mechi tatu hakuwepo kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Yanga ilishinda kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana jambo ambalo limeifanya Yanga kutwaa taji la pili la Kombe la Mapinduzi.

Mchezo wa fainali ulichezwa Uwanja wa Amaan ulishuhudiwa na mashabiki wengi waliojitokeza kuona mechi iliyokuwa na ushindani mkubwa.


Saido amesema:"Wachezaji wenzangu huwa ninawakubali na wao wananikubali, sasa walipoona mimi nipo na ninaweza kazi wakaniambia twende nami nikafanya kazi.

"Mchezo wangu dhidi ya Simba nilicheza licha ya kwamba bado nilikuwa nina maumivu ila nilifanya kwa ajili ya kazi na uwezo wangu mimi ni kucheza," . 

Yanga inatarajiwa kurejea leo na Kombe la Mapinduzi ambalo wamelitwaa visiwani Zanzibar.

8 COMMENTS:

  1. Huyi mrundi nae kelele nyingi. Aliomaliza simba kwa mpira gani aliocheza? Wakati mwingine kukaa kimya kunakupa heshima, sio kila siku unajitapa unadhani mchezaji wa maaana kumbe wa kawaida tuu. Mchezaji wa maana hasajiliwi akiwa huru

    ReplyDelete
  2. Saido aliimaliza Simba baada ya kufunga mabao mangani ndani ya dakika alizocheza ambazo zilikuwa ndani ya dk 90 za mchezo?

    ReplyDelete
  3. MUACHENI PIGE KELELE AKAE AJUWE KUWA HAJACHEZA HATA MECHI 10 HAPA, AMEANZA KUUMWA

    ReplyDelete
  4. Hovi saido ana miaka mingapi mbona kibabu mno?

    ReplyDelete
  5. Acha kumsema kwani jioni serious yake kwà mechi chache najua wengi gumuuu Kuna Wana Simba hawataki madanikio ya Yanga na Yanga hawaja elewa Wana chichewa tuuu na Wana Simba

    ReplyDelete
  6. Ntinazonkiza tupo juuu aches kusema neno na uonho eti hawezi Kama hawezi nenda Wewe kachezeee uone Kama Sio utumbo ukiwa nje unaona Sana sasabingia ndani

    ReplyDelete
  7. kacheza mpira gani huyoo boyaa
    kaimaliza labda kwa hiyoo penalty yake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic