UONGOZI Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa upo kwenye hesabu za kumtafuta mbadala wa nyota wao Dickson Job ambaye yupo zake ndani ya kikosi cha Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi Yanga.
Job amesaini dili la miaka miwili ndani ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze kwa sasa nafasi yake imebaki wazi ndani ya Mtibwa Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa kwa kuwa mchezaji ameondoka wao wanasubiri kuona mapendekezo ya benchi la ufundi kisha wafanyie kazi.
"Ukizungumzia Mtibwa Sugar hapa ni chuo cha kulea na kukuza vipaji, tunachokifanya kwa sasa ni kuangalia ripoti ya kocha na mapendekezo yake kisha tunayafanyia kazi.
"Ikiwa tutashindwa kupata mchezaji mpya kwa sasa tunao vijana pale Mtibwa Sugar wapo vizuri tutawapandisha na watafanya kazi kwa uhakika hatuna mashaka na uwezo wao.
"Wale vijana wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki jambo ambalo linatufanya tuwe imara muda wote na tufanye kazi kwa ushirikiano," amesema.
Job ambaye alikuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ambayo imekwenda kushiriki michuano ya Chan, amebaki Bongo kwa kile kilichoelezwa kuwa alipata majeraha.
Karibu sana kwenye Chama la WANANCHI Djob
ReplyDelete