January 15, 2021


IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Tottenham ipo tayari kuingia kwenye ushindanai na Klabu ya Chelsea kwenye kuwania saini ya beki wa kati raia wa Korea Kusini Kim Min-jae.

Jose Mourinho, Kocha wa Tottenham anaamini kuwa ikiwa atampata beki huyo atakuwa imara kwenye safu yake ya ulinzi jambo linalomfanya asiwe na mashaka katika kusaka saini ya nyota huyo.

Beki huyo anatajwa kuwa pia kwenye hesabu za Chelsea ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya Klabu ya Beijing Guuoan na mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu wa mwaka 2021.

Mourinho tayari anatajwa kuanza mazungumzo na mabosi wa nyota huyo mwenye miaka 24 ili kuweza kupata huduma yake ndani ya kikosi chake ambacho kinashiriki Ligi Kuu England.

Anaungana na mabosi wake wa zamani wa Chelsea ambayo ipo chini ya mwanafunzi wake wa zamani Frank Lamapard ambao nao wanatajwa kuwa kwenye hesabu za kuinasa saini ya Mkorea huyo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic