IMEELEZWA kuwa nyota wa kikosi cha Barcelona, Lionel Messi ameanza kujifunza Lugha ya Kifaransa na anahusishwa pia kuwa kwenye hesabu za Klabu ya PSG.
Mkataba wa mshambuliaji huyo ndani ya Barcelona unameguka mwishoni mwa msimu huu na amekuwa akitajwa kuhitaji kupata changamoto mpya.
Pia amekuwa akiwaambia mabosi wake wa Barcelona kwamba wamrejeshe kundini mshkaji wake Neymar Jr ambaye yupo ndani ya Klabu ya PSG.
Kuanza kwake kujifunza Kifaransa kunatajwa kuwa maandalizi ya raia huyo wa Argentina kuanza kuifukuzia ndoto yake ya kucheza na rafikiye Neymar Jr.
Mabosi wa Barcelona wamekuwa wakipambana kuhakikisha kwamba nyota huyo anabaki ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki La Liga.
Msimu huu mambo yameonekana kuwa magumu kwa Messi ambapo ametupia jumla ya mabao 14 kwenye mechi 22 ambazo amecheza mpaka sasa kwenye michuano yote.
Pia kwa sasa hali ya uchumi wa Barcelona imeyumba ambapo inaelezwa kuwa mpaka kufika Juni 2021, benki kutakuwa kuna kiasi cha shilingi bilioni 756 jambo linalomaanisha kwamba mambo ni magumu huku ikielezwa kuwa mshahara wa mwezi Desemba haijawalipa wachezaji wake mshahara.
0 COMMENTS:
Post a Comment