SALUM Abubakar, kiungo wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa bado wana imani ya kuweza kufikia malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara uliopo mikononi mwa Simba.
Kwenye msimamo msimu wa 2020/21 Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ipo nafasi ya tatu ina pointi 32 baada ya kucheza mechi 17.
Kinara kwenye msimamo ni Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18 za Ligi Kuu Bara.
Mabingwa watetezi Simba wamejichimbia nafasi ya pili na pointi zao ni 35 baada ya kucheza mechi 15.
Kwenye Kombe la Mapinduzi, Azam FC ilitolewa hatua ya nusu fainali na Yanga kwa kufungwa penalti 4-3, Uwanja wa Amaan.
Kwa sasa imeweka kambi Visiwani Zanzibar ikiwa ni maandalizi ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la FA.
Sure Boy amesema:"Bado malengo yetu yapo palepale, kushindwa kupata matokeo kwenye mechi zetu za nyuma haina maana kwamba tumetoka kwenye reli bado tunahitaji kuona tunatwaa ubingwa na kila kitu kinawezekana,".
Huyu nae anaota wenzao simba yanga wanasajili majembe wao na monzizi tu na kipa,,,huwezi kupata ubingwa na kiungo kama huyo nionzima wao,,,legelege hatari
ReplyDelete