January 23, 2021


BAADA ya kupoteza mchezo wake wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Zambia wachezaji wamekubaliana kucheza mchezo wa leo kama fainali dhidi ya Namibia.

Leo Januari 23 Taifa Stars itakuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Namibia na mchezo wake wa mwisho itakuwa ni Januari 27 dhidi ya Guinea.

Ikiwa kundi D, ipo nafasi ya tatu na haijakusanya pointi huku nafasi ya kwanza ikiwa mikononi mwa Guinea na ya pili ni Zambia zote zina pointi tatu huku Namibia ikiwa nafasi ya nne bila pointi.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Clifford Ndimbo amesema kuwa wachezaji wamekubaliana kucheza mchezo wao dhidi ya Namibia kama fainali.

“Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Zambia, wachezaji wamekubaliana kucheza mchezo wetu dhidi ya Namibia kama fainali pia hata ule dhidi ya Guinea pia hali itakuwa hivyo kwa kuwa malengo ni kupata ushindi na kutinga hatua ya robo fainali,” amesema.

 Muda wa mchezo utakuwa saa 2:00 kwa saa za Cameroon ila kwa Tanzania itakuwa saa 10:00 usiku, Uwanja wa Limbe na wanaotarajiwa kuukosa mchezo wa leo ni pamoja na mshambuliaji John Bocco na beki Ibrahim Ame pamoja na Erasto Nyoni ambao wapo chini ya uangalizi wa jopo la madaktari kwa kuwa wanasumbuliwa na majeruhi.

7 COMMENTS:

  1. Saa 10 usiku...!!??? Hebu tuwekeni sawa jamani

    ReplyDelete
  2. sku zote sisi wasindikizaji tu sijaona kipya mpaka sasa. kocha anaita wachezaj wageni kwenye ashindano wakiachwa wazoefu huo si utani kabisa. mwsho wa sku short on target 1 tu ndani ya dakika 90 na hapo tunategemea tuqualify,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hao wachezaji wazoefu wamefanyann hadi sasa toka wanaichezea timu ya bado tupokulekule tu kwawasiojua

      Delete
  3. Kwanini hao majeruhi walienda na wachezaji waziri wengine wapo?

    ReplyDelete
  4. Juma nyoso mbona ni beki nzuri wa Kati kwa nini hachaguliwi

    ReplyDelete
  5. Juma nyoso kwa nini haitwi Taifa star mbona ni beki nzuri wa Kati na pia anauzoefu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic