KLABU ya Coastal Union iko kwenye nafasi nzuri ya kumnyakua mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Waziri Junior kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili.
Waziri ameonekana kuwa na wakati mgumu ndani ya kikosi cha
Yanga ambapo mpaka sasa ameifungia bao moja pekee, huku kiwango chake
kikionekana kuwapa maswali mengi mashabiki na viongozi wa klabu hiyo.
Coastal hawako wenyewe katika vita hiyo kwani inatajwa kuwa
Ihefu nao wamekuwa wakimkimbizia nyota huyo.
Juma Mgunda kocha mkuu wa Coastal Union anaamini kuwa akimpata mshambuliaji mzoefu atafanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara.
Waziri akiwa na Mbao msimu uliopita alifanikiwa kumaliza
katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa wafungaji baada ya kuweka kambani mabao
13, kiasi cha kuishawishi Yanga kumsajili lakini anaonekana kupitia wakati
mgumu msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment