January 24, 2021


 FARID Mussa kiungo wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, usiku wa kuamkia leo aliwamaliza Namibia kwa kuwatungua bao moja na kusepa na tuzo ya mchezaji bora wa mchezo.

Stars imeshinda mchezo wake wa kwanza kwenye mashindano yanayohusisha wachezaji wa ndani,Chan na kuipa pointi tatu muhimu Stars.

Mchezo wa kwanza Stars ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Zambia ambayo nayo ililazimisha sare mbele ya Guinea na kukusanya jumla ya pointi nne.

Mussa alitupia bao la ushindi dakika ya 65 na kuifanya Namibia kuyeyusha mazima pointi tatu, kituo kinachofuata ni dhidi ya Guinea, Januari 27.

Hata hivyo hakumaliza dakika zote 90 uwanjani kwa kuwa alitoka dakika ya 88 kumpisha kiungo  Baraka Majogoro ambaye alikwenda kumalizia dakika zilizobaki.

Kwenye mchezo huo pia wachezaji walisimama kwa muda baada ya taa za Uwanja wa Limbe, Cameroon kuzima ghafla.

Stars inakuwa nafasi ya tatu huku Namibia ikiwa imeshaaga mashindano jumla matokeo ya mchezo wa mwisho yataamua nani atakuwa nani kwenye kundi hili D.

6 COMMENTS:

  1. Hongera.. matunda ya Azam fc yanaonrkana pole pole.. japo yanga hawaoni umuhimu wako.. we sepa tu katafute timu hata morocco

    ReplyDelete
    Replies
    1. Maneno ya kichochezi hayo. Kwani kule Yanga hachezi na hathaminiwi? Usianze kupandikiza chuki

      Delete
  2. Mbona nyie kwenu wenye vpaj na hawathaminiw ni weng tu au kisa kawa yanga ndo unawashwa?

    ReplyDelete
  3. Tunamwangalia ,Jana wachrzaji wa yanga wa 5 ndani tumeshinda ongeza na huyo moja tuwape Guinea 2 amini

    ReplyDelete
  4. Achaneni usimba na Uyanga, haijalishi wasimba wamecheza wangapi au wayanga wamecheza wangapi wote si watz

    ReplyDelete
  5. Tanzania ndio inacheza CHAN. Ila mashabiki sasa ambao hata huko ilikokwenda timi yao hawajaenda,wanajua kumlaumu na kuiombea mabaya. Jamani Ligi Kuu sio mwisho wa soka la wachezaji. Lazima waende zaidi ya hapo na wakosee nawapatie. Kikubwa ni kuleta mawazo ambayo shirikisho letu likubali kuyafanyika kazi ili kikosi cha Taifa nacho kiwe imara na thabiti.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic