January 19, 2021

 


KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije leo kimeanza kwa kupoteza mbele ya Zambia.

Dakika 45 zilikamilika kwa timu zote kumaliza bila kufungana huku Stars ikionekana kupata nafasi za wazi na kushindwa kuzitumia kupitia kwa nyota Ayoub Lyanga ambaye aliumia kipindi cha pili.

Bao la kwanza kwa Zambia ya Micho ambaye aliwahi kuinoa Yanga zamani lilipachikwa na Collins Sikombe kwa mkwaju wa penalti dakika ya 64.

Penalti hiyo ilipatikana katika harakati za kuokoa ambapo Kapombe Shomari alinawa mpira wakati akiokoa hatari akiwa ndani ya 18 na alionyeshwa kadi ya njano ikiwa ni ya kwanza kwa Stars.

Bao la pili lilifungwa na Emmanuel Chabula dakika ya 80 kwa shuti kali ambalo lilimfanya Aishi Manula asiwe na la kufanya.

Nyota wa Zambia, Sikombe amekuwa mchezaji bora wa mchezo baada ya kufunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao kwenye mchezo wa leo. 

Pia ikiwa ni mara ya pili kwa timu ya Taifa ya Tanzania kushiriki Chan ilianza 2009 pia ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Senegal hivyo rekodi imejirudia mwaka huu.

17 COMMENTS:

  1. .. kwa hii timu ya Taifa Stars iliyicheza, inafungwa hata na Simba SC Kama tulipanga timu yetu vizuri. Hii ni pamoja na kuwaachia Kapombe naanula halafu tupange kikosi chetu. Kwa maana hiyo hatuna kocha kwa kweli!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama huna uwezo wa kutoa commenti ni afadhali kukaa kimya!

      Delete
    2. Wewe umeona Kuna kocha pale, Au kwa sababu nimeitaja Simba?

      Delete
  2. Replies
    1. Kafundishe timu yako ya mitaani, siyo kila kinachokujia kichwani unakitoa tu. Hata ku-comment maswala ya mpira un'abitazione kufikiri

      Delete
  3. Kukosa uzoefu wa mechi za kimataifa kwa baadhi ya wachezaji wetu kumeigharimu timu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani kocha ana uzoefu wa kimataifa?

      Delete
    2. Kwani kuna ulazima gani wa kujaza lundo la wachezaji wasiokuwa na uzoefu na mechi za kitaifa na kuwaacha wenye uzoefu?Hii ni dhahiri kuwa kocha, mkurugenzi na benchi lote la ufundi ni dhaifu,hawana uzoefu na wako kama wanajifunza.TFF iache kutuletea makocha wa majariio na wa bei chee.Mie Kwangu ni bora hata Boniface Mkwasa,Babu Hans Plujim.
      Unaenda kucheza mechi za kimataifa ndani ya week mbili halafu kocha unaokota-okota nusu ya wachezaji hawana uzoefu wa kimataifa.Utamuachaje Mohammed Hussein, Metacha Mnata,Suleiman Nado, Abubakary Salumu,Mzamiru,Jonas Mkude...Kwa biashara ya TFF tutaendelea kuwa washiriki na si washindani.

      Delete
  4. Bora hata Mbeya City ingeweza kutoa ushindani lakini sio kwa timu hii

    ReplyDelete
  5. Yanga Damu anapinga ukweli kuwa Mnyama anaweza kuifunga timu ya taifa, yeye alitaraji kusikia kuwa hata yanga ingeweza kuifunga timu ya taifa

    ReplyDelete
  6. Tunatia aibu kw washambuliaji kushindwa kupachika magoli

    ReplyDelete
  7. Hapo bado kwa wale Guine wanaupiga mwingi

    ReplyDelete
  8. Tunavuna tulichopanda, kama wachezaji hawafuati Maelekezo ya Coach hata umlete Zidane hatuifikidha popote team ya Taifa stars, kwakifupi wachezaji wetu ndio tatizo.
    Bado tunasafari ndefu kufikia level ya kutambulika kimataifa

    ReplyDelete
  9. Mechi ijayo tunacheza na nani, lini, na saa ngapi? Waandishi mnakwama wapi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic