January 19, 2021


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa bado haujaachana na mchezaji wao Michael Sarpong ambaye kwa sasa ameelekea nchini China kwa ajili ya majaribio.

Sarpong aliibuka ndani ya Yanga akitokea nchini Rwanda ambapo alikuwa anacheza Klabu ya Rayon Sports ila yeye ni raia wa Ghana.

Ndani ya Yanga inayonolewa na Cedric Kaze ametupia mabao manne kati ya mabao 29 katika mechi 18 ikiwa ipo nafasi ya kwanza na pointi zao ni 44.

Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa kuachana na mchezaji kwa wakati huu sio jambo jepesi hivyo watu wasifikirie kwamba nyota huyo ameachwa.

“Unafikiri kuachana na mchezaji ndani ya Yanga ni kitu chepesi? Hilo halipo kuna utaratibu ambao upo na kwa sasa mchezaji bado ni mali ya Yanga kwani hata hayo majaribio nchini China bado hajafanya,” alisema Mwakalebela.

Nyota huyo alikuwa miongoni mwa wale ambao walishiriki Kombe la Mapinduzi ambapo walishinda mbele ya Simba kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic