January 15, 2021

 



KLABU ya Black Leopards ya nchini Afrika Kusini ipo kwenye mipango ya kukamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Tanzania aliyewahi kukipiga na klabu za Simba na Coastal Union, Abdi Banda.

Banda ambaye alikuwa nje kwa muda kufuatia kupata majeraha ya goti amepewa mwaliko na uongozi wa Leopards, wa kufanya nao mazoezi kwa muda wa wiki mbili ili kujihakikishia utimamu wa mwili baada ya kupona majeraha.

Banda amebakisha mwaka mmoja pekee katika mkataba wake na Highlanders inayommiliki na tayari Leopards wamekwishaanza mazungumzo ya kuvunja mkataba huo.

Akizungumzia usajili huo, Banda alisema: “Ni kweli uongozi wa Leopards umenitumia mwaliko wa kufanya nao mazoezi kwa muda wa wiki mbili, ili kuangalia kama nina utimamu wa kutosha wa mwili baada ya kutoka kwenye majeraha ya goti.

“Kwa sasa mkataba wangu na Highlanders umesalia na muda wa mwaka mmoja pekee na tayari viongozi wa Leopards wameonyesha nia ya kunipa mkataba kwani wamekubali kuanza mazungumzo ya awali,”

7 COMMENTS:

  1. Kwani huyu bado ni beki was Simba?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Rogatus, huu ndio ukanjanja wa watu hawa wanaojiita 'waandishi'. Inakera kweli!

      Delete
  2. Ila saleh jembe unashindwa tu kutumia Jina la timu anayochezea kwa wakati huo mpaka utaje timu kubwa ili watu wasome au

    ReplyDelete
  3. Angeandika beki w zamani wa simba

    ReplyDelete
  4. Jamani njaa mbaya msimlaumu sana jembe mwache andelee kutuibia mb zetu kwa kuandika habari za ukanjanja

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic