NEEMA imezidi kuwashukia wasomaji wa Gazeti la Spoti Xtra ambalo linazidi kutoa zawadi mbalimbali kupitia chemsha bongo inayoendeshwa na gazeti hilo kwa kushirikiana na Kampuni ya Vunja Bei Mobile Shop ambao ni wauzaji wa vyombo vya majumbani.
Wiki hii washindi wawili, Emmanuel Ndetaulwa Issangya mkazi wa Mwananyamala Kisiwani na Irene Deogratius Michael wa Tabata Kinyerezi, kila mmoja alijishindia tea set baada ya kujibu kwa ufasaha swali lililouzwa ndani ya Gazeti la Spoti Xtra.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake leo Ijumaa katika Ofisi za Gazeti la Spoti Xtra zilizopo Sinza Mori, Dar, Irene alisema: “Nashukuru Gazeti la Spoti Xtra kwa zawadi hii, mwanzoni nilikuwa nadhani ni uongo lakini baada ya kuibuka mshindi nimeamini kuwa zawadi hazitolewi kwa upendeleo.
“Napenda kusoma Spoti Xtra kutokana na habari za uhakika ambazo zinaandikwa pia napenda kusoma hadithi zilizopo humu ndani, nawashauri Watanzania wenzangu wasome Gazeti la Spoti Xtra, pia washiriki chemsha bongo na wao watabahatika siku moja.
“Mimi ni shabiki wa Yanga, ninampenda zaidi Saidi Ntibazonkiza na Tuisila Kisinda. Habari za Yanga na timu nyingine huwa nazikuta ndani ya Spoti Xta zikiwa zimeandikwa kwa umahiri mkubwa sana.”
Naye Emmanuel ambaye ni shabiki wa Simba, alisema: “Mimi ni mdau mkubwa wa magazeti ya Spoti Xtra kutokana na ubora wake na aina ya habari zinazoandikwa ni za kweli.
“Mwanzoni nilikuwa siamini kama mtu anaweza kushinda kweli lakini baada ya kujishindia zawadi hii nawaomba na wasomaji wengine wasikate tamaa, wazidi kusoma Gazeti la Spoti Xtra ili waweze kujishindia zawadi.”
Kwa upande wa Mhariri wa Gazeti la Spoti Xtra, Omary Mdose, alisema: “Tunawashukuru washirika wetu Kampuni ya Vunja Bei Mobile Shop ambao ndiyo wadhamini wa chemsha bongo inayoendeshwa kwenye Gazeti la Spoti Xtra.
“Nawaomba wasomaji wazidi kusoma gazeti hili kwani kwa hapa Tanzania, ndiyo gazeti ambalo linaongoza kwa kuandikwa takwimu nyingi za michezo mbalimbali huku zikiwa na habari za kina zilizohaririwa kwa umahiri mkubwa.
"Spoti Xtra linapatikana mtaani kwa Sh 500 na linatoka mara tatu kwa wiki, JUMANNE, ALHAMISI na JUMAPILI. Ukifungua ukurasa wa pili, utakutana na maelekezo ya namna ya kushiriki chemsha bongo ambayo itakuweka karibu kuwa mshindi.”
Mtangazaji wa +255 Global Radio na Global TV Online ambaye pia ni mwakilishi wa Kampuni ya Vunja Bei Mobile Shop, Kissa Daniel, amesema: “Vunja Bei Mobile Shop kwa kushirikiana na Spoti Xtra tumeendelea kutoa zawadi mbalimbali kwa wasomaji wetu, ambapo linawapa fursa ya kujishindia vitu mbalimbali ikiwemo friji, Brenda, seti ya vyombo na vingine vingi. Kikubwa wasomaji wazidi kusoma gazeti hili ili wapate fursa ya kuibuka na zawadi kemkem.”
Gazeti la Spoti Xtra kwa kushirikiana na Vunja Bei Mobile Shop, imeanzisha chemsha bongo hiyo yenye lengo la kuwaleta karibu wasomaji wake huku pia ikiwa ni ujio wa Gazeti la Spoti Xtra Jumanne lililoanza kuingia mtaani Desemba 17, mwaka jana. Awali Spoti Xtra lilikuwa likitoka Alhamisi na Jumapili, lakini sasa imeongezeka Jumanne.
0 COMMENTS:
Post a Comment