January 22, 2021


 KAMATI ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi imetangaza kuwa mapato ya mchezo wa fainali kati ya Yanga na Simba ni milioni 79 na laki mbili na elfu arobaini na tano.

Fainali hiyo ya Mapinduzi ilichezwa Visiwani Zanzibar, Januari 13,2021 na Simba kushuhudia Yanga ikisepa na taji la kwanza kwa mwaka 2021.

Yanga ilishinda kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Amaan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Kamati hiyo, Bibi Imane Duwe amesema jumla ya Shilingi Milioni 496, laki 1, elfu 78 na mia 4 wamekusanya katika mashindano kutoka kwa Wadhamini na Viingilio vya milangoni ambapo baada ya kulipa matumizi yote wanatarajia kubakisha Shilingi Milioni 141, laki 7 na elfu 3 ambazo watazirejesha Serikalini.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Yanga kusepa na taji la Mapinduzi huku Simba ikiwa imefanikiwa kutwaa taji hilo mara tatu.

Vinara wa kutwaa taji hilo ni Azam FC ambao wametwaa mara tano taji la Mapinduzi na mwaka 2021 waliishia hatua ya nusu fainali baada ya kutolewa na mabingwa Yanga.

1 COMMENTS:

  1. Kwa io walikua bado wanahesabu hizo hela ndo wamemaliza leo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic