DIRISHA la usajili lilifungwa rasmi Ijumaa usiku na kushuhudia timu za Simba na Yanga zikishusha wachezaji wapya na kuwatambulisha ikiwa umebaki muda mchache kabla ya dirisha hilo kufungwa.
Yanga ilifunga usajili wao kwa kuutambulisha usajili wa
mshambuliaji wao mpya mwenye uraia wa Burundi, Fiston Abdoul Razak huku Simba
wao wakimaliza na kiungo mshambuliaji raia wa Zimbwambwe Tatenda Perfect
Chikwende.
Kutokana na sajili hizo viongozi wa pande zote mbili
wameibuka huku kila upande ukijinasibu kuwa kwenye mawindo yake Simba
ikijinasibu kwenda kimataifa huku Yanga wao wakitamba kusepa na kombe la Ligi Kuu.
Mjumbe wa kamati ya usajili wa Yanga Injinia Hersi Said yeye
amesema: “Tumekamilisha usajili wa maboresho ndani ya dirisha dogo la usajili
kwa lengo la kuushinda kombe la Ligi Kuu msimu huu,”
Kwa upande wa Simba Ofisa mtendaji mkuu (CEO) wa timu hiyo Barbara Gonzalez yeye amesema
kuwa “Usajili wa Perfect Chikwende ni kwa ajili ya kuiongezea nguvu timu yetu
katika safu ya ushambuliaji kuelekea katika michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika
ambayo tumetinga hatua ya Makundi,”
Wamchangani usajili niwakimchachanga tu na wakimataifa usajili niwakimataifa
ReplyDeleteWe kweli kilaza, kati ya Fiston na Chikwende nani mwenye CV kali?
DeleteMchezaji anaangaliwa current performance yake ikoje, CV waachie makocha... Mliangalia CV ya Sarpong ona sasa anakimbiakimbia tu uwanjan
DeleteKwa yivyo injinia Hersi yupo kimatopeni zaidi?
ReplyDelete