January 17, 2021

 


KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije amesema kuwa ana matumaini makubwa kwamba kikosi chake kitaanza vizuri kampeni ya michezo ya CHAN inayofanyika nchini Cameroon kwa kuifunga timu ya Taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’.

Stars tayari imetua nchini Cameroon na kikosi cha wachezaji 27 kwa ajili ya michuano hiyo huku mchezaji wa klabu ya Simba, Erasto Nyoni na kocha Seleman Matola wakiwa njiani kujiunga na kikosi hicho baada ya kumaliza majukumu yalikuwa yakiwakabili.

Kikosi cha Stars kimepiga kambi katika Jiji la Limbe kikiendelea na mazoezi katika uwanja wa Centenary, kujiandaa na mchezo wa kwanza wa kundi D dhidi ya Zambia utakaopigwa kesho kutwa Jumanne, kabla ya kucheza mchezo wa pili dhidi ya Namibia Januari 23 na kumalizia na Guinea Januari 27.

Akizungumzia kuhusu maandalizi yao, Ndayiragije amesema: “Tunashukuru kwa kuwasili salama nchini Cameroon kwa ajili ya michuano hii ya CHAN ambapo tayari tumeanza mazoezi ya kujiandaa na michezo yetu ya kundi D, hasa ule wa ufunguzi dhidi ya Zambia ambao ni muhimu zaidi tukashinda ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushinda michezo yetu inayofuata,”

 

 

7 COMMENTS:

  1. Hamna kitu hapo, mswahili ni huyohuyo na kanzu yake, goli 3 zinatusubiri

    ReplyDelete
  2. Hizo ni ndoto zako ila sisi tunaamini tumenda kushindana matokeo mazuri tutayapata tu hao majirani zetu tunawanyosha tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kocha wenu na swahiba wake wana nini zaidi ya hapo?

      Delete
  3. mechi zetu zote ni ngumu sana tu, sasa sielewi kipi kinampa jeuri ya kusema et ana matumaini kibao, au mechi ya kirafiki ya CONGO hahaha

    ReplyDelete
  4. Lolote linawezekana, zaidi ya yote wachezaji wanatakiwa wapambane.

    ReplyDelete
  5. Itavokuwa, ni lazema tuitakie heri Tanzania bila kukejeli chetu. Yanga ilifanya uungwana wa hali ya juu ilipokuja Platinum ya Zimbabwe tulikuwa sote mkono mmoja na matokeo tunayaona na moyo huo uendelee nao na kubana chuki zetu hata wageni wakatucheka na wao kupata ushindi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic