January 29, 2021

 


OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa msanii Zuchu ambaye anafanya vizuri na ngoma yake ya sukari atatumbuiza kwenye kilele cha Simba Super Cup.

Mashindano ya Simba Super Cup yameanza Januari 27 ambapo yanashirikisha timu tatu ambazo ni Simba wenyewe wakiwa wenyeji, Al Hilal na TP Mazembe ambazo zinachezwa  leo Uwanja wa Mkapa.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ilianza kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal Uwanja wa Mkapa.

Januari 31 itakuwa ni kilele cha Simba Super Cup ambapo Zuchu atatumbuiza siku hiyo.

Pia Simba itamaliza kwa kucheza na TP Mazembe ya Congo, Uwanja wa Mkapa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic