MCHEZO wa kirafiki kati ya Azam FC dhidi ya TP Mazembe leo Februari 2,2021 umekamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu George Lwandamina ilianza kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Never Tigere ambaye alifunga kwa mpira wa faulo akiwa nje ya 18.
Tigere aliweza kufanya majaribio matatu ambayo yalikwenda nje ya lango na faulo yake aliyopiga ilimshinda mlinda mlango namba moja wa TP Mazembe Muonkoro Ibrahim ambaye alikuwa kwenye ubora wake.
TP Mazembe inayonolewa na Kocha Mkuu, Isaac Kasogo ambao walianza na Mtanzania, Thomas Ulimwengu ambaye hakumaliza dakika 90 waliweka usawa baada ya dakika tatu kupitia kwa Adam Boso dakika ya 71 baada ya kuwashinda mbinu mabeki wa Azam FC.
TP Mazembe inafanikiwa kucheza mechi mbili mfululizo kwa timu za Bongo bila kupoteza ambapo ilipata sare dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Simba Super Cup na leo mbele ya Azam FC Uwanja wa Azam Complex dhidi ya Azam FC.
Azam FC inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba ambao ni wa kiporo unaotarajiwa kuchezwa Februari 7, Uwanja wa Mkapa na TP Mazembe ipo hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment