February 2, 2021

 


HATIMAYE Jonas Mkude amerejea kikosini kuungana na wachezaji wenzake baada ya kumaliza kuitumikia adhabu yake kutokana na utovu wa nidhamu.


Mkude leo Februari 2 ameanza mazoezi na wachezaji wenzake baada ya kusimamishwa na Kamati ya nidhamu ya Simba Desemba 28,2020.


Tayari alikuwa amekosekana kwenye jumla ya mechi nane ambazo Simba walicheza ndani ya uwanja, zama zile za Sven Vandenbroeck alikosekana kwenye mechi tatu ndani ya uwanja.


Moja ilikuwa ya Kombe la Shirikisho,  moja ya Ligi ya Mabingwa Afrika na moja ilikuwa ya Ligi Kuu Bara kabla hajabwaga manyanga Januari 7 na kuibukia Morocco. 


Ikiwa chini ya Kaimu Kocha, Seleman Matola amekosekana kwenye mechi nne ilikuwa ni za Kombe la Mapinduzi,  Visiwani Zanzibar ambapo mabingwa ni Yanga baada ya kushinda kwa penalti 4-3 dhidi ya Simba kwenye fainali iliyochezwa Uwanja wa Amaan.


Mbele ya Didier Gomes mrithi wa Sven amekosekqna kwenye mechi mbili za Simba Super Cup ambapo aliwakosa Al Hilal na TP Mazembe na mabingwa wakawa Simba.


Jumla amekosekana kwenye mechi nane za Simba ndani ya uwanja kiungo huyo mkabaji kipenzi cha mashabiki.


Ofisa Habari wa Simba,  Haji Manara amesema kuwa Mkude ni mchezaji wa Simba na makosa ambayo aliyafanya ni ya kibinadamu.

4 COMMENTS:

  1. Jana imeandika kuwa wachezaji wenzie wamegoma asirudi mpaka mechi kumi zipite kweli we juha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ameshatumikia zaidi ya nusu ya adhabu aliyopewa kwa hiyo anastahili kurudi kundini,mechi mbili zilizobaki ni theluthi ndogo sana.Uwe unatingisha ubongo wako kabla ya kukurupuka kudhihaki wenzako.

      Delete
  2. Inshalla iwe funzo na iliyobaki Mkude jiti na macho baba ujijaalie umekaa juu ya tawi kavu ukianguka hapana tena wa kukuokota na kukupa pole na talaka zikishafika tatu ndio kwa heri ya kuonana

    ReplyDelete
  3. ANACHEZA NAMBA YA NAN LWANGA YPO GOOD

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic