February 27, 2021


 BRUCE Kangwa, nahodha msaidizi wa kikosi cha Azam FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Mbuni FC utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Mbuni ili iweze kutinga hatua ya 16 bora.

Akizungumza na Saleh Jembe Kangwa amesema kuwa wapo tayari na wanaamini watafanya vizuri ndani ya dakika 90 licha ya kutuwajua aina ya uchezaji wao ndani ya uwanja.

"Kiujumla wachezaji wapo tayari na kila kitu kuhusu maandalizi kipo sawa hivyo mashabiki watupe sapoti ndani ya uwanja.

"Wapinzani wetu kiukweli hatuwajui namna ambavyo wanacheza ila tutacheza nao kama fainali kwa kuwa tunajua kwamba timu ndogo zinatoa timu kubwa hilo tunalijua tutapambana ili tusipate matatizo,".

Jana kikosi hicho kilifanya mazoezi ya mwisho ndani ya Uwanja wa Azam Complex huku kipa wao Martin Kingonya akionyesha uwezo na huenda akaanza leo mbele ya Mbuni FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic