February 27, 2021

 


JUNIOR Lokosa, mshambuliaji mpya ndani ya kikosi cha Simba anatajwa kuwa kwenye hesabu za timu moja ya nchini Norway ambayo inahitaji huduma yake.

Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes, Lokosa bado hajapata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kwenye mechi 8 ambazo Gomes ameziongoza msimu wa 2020/21.

Habari zinaeleza kuwa bado Gomes hajaelewa uwezo wake hivyo itakuwa rahisi kwa raia huyo wa Nigeria mwenye miaka 27 kusepa mazima ndani ya kikosi hicho baada ya kusaini dili la miezi sita.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wachezaji ambao wamesajiliwa na Simba huwa inawachukua muda kuingia kikosi cha kwanza hivyo wale ambao wanambeza Lokosa wataona uwezo wake.

"Lokosa ni moja ya wachezaji wazuri na ataingia kwenye mfumo hivi karibuni hivyo kama kuna watu ambao wanambeza basi wasubiri pale atakapojibu ndani ya Simba.

"Kuhusu biashara ya wachezaji tunajua kwamba wachezaji wanahitajika na wapo mawakala ambao wanahitaji huduma zao hapo sasa ni suala la dau kuangalia namna itakavyokuwa," .

4 COMMENTS:

  1. Huyi hajawahi hata kuonekana itakuwaje auzwe? Anakula mshahara wa bure tuu bora aondoke

    ReplyDelete
  2. Maana ya kutaka kikosi kipana ndo matokeo yake hayo,imekuwa kama kokoro linakusanya kila kitu ilimradi tu watu wapige cha juu

    ReplyDelete
  3. Mtambo wa mabao kafunga mangapi huyu?

    ReplyDelete
  4. Hata Lwanga watu walibeza. Simba bado ana mechi nne mkononi kwenye hatua ya makundi. Na atakuwa na mechi kadhaa za kucheza Kama Simba atatinga robo na nusu fainal. Kwa hivyo sioni sababu ya watu kuanza kuwa na viharahara vya mdomo kuhusu Lukosa na wachezaji wengine waliosajiliwa kwa ajili ya klabu bingwa. Kuhusu Lukosa muda utaongea ila nnaamani ndie mchezaji atakaeipeleka simba mbali klabu bingwa.Simba hivi karibuni wamekuwa na tamaduni nzuri ya kuwapa muda wachezaji wao waliokuwa hawapo fiti kurejea taratibu kwenye ubora wao. Hata chikwende watu walishaanza kumbeza na siamini ni Mashabiki wa Simba ni utopolo.Ukiangalia Sarpong wa Yanga anaecheza kila siku lakini bora hata huyo lokosa aliekaa benchi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic