February 28, 2021


 WAZIR Junior mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa anachopitia kwa sasa ni suala la muda ana amini kwamba atapata nafasi ya kucheza.

Kwenye usajili wa dirisha dogo, timu zaidi ya tano ikiwa ni pamoja na KMC, Coastal Union, Gwambina na Namungo zilikuwa zinahitaji huduma yake kwa mkopo ia dili lake libuma baada ya Kocha Mkuu,Cedric Kaze kuhitaji huduma yake.

Junior ambaye ni ingizo jipya kutoka Klabu ya Mbao FC bado hajawa na nafasi kikosi cha kwanza zaidi ya kujenga ushkaji na benchi.

Nyota huyo amesema:"Ilikuwa niondoke wakati ule wa dirisha dogo ila mwalimu alitaka nibaki hivyo nina amini kwamba bado nina nafasi ya kufanya vizuri.

"Kikubwa ni kuendelea kupambana ili kuwa bora kwa kuwa ushindani ni mkubwa na kila kitu nina amini kwamba kila kitu kitakuwa sawa,".

Ndani ya Yanga ametupia bao moja ilikuwa mbele ya KMC wakati Yanga ikishinda 2-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic