February 2, 2021

 



UBORA wa kikosi cha Simba hasa baada ya kushusha majembe ya kazi ikiwemo Mzimbabwe Tatenda Perfect Chikwende, na kurudi kwa makali ya, Bernard Morrison kumemshtua kocha wa Azam, George Lwandamina ambaye ameongeza msisitizo wa program za mazoezi ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Simba.

Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa Simba na Azam kukutana msimu huu ambapo unatarajiwa kupigwa Februari 7, mwaka huu ukiwa sehemu ya michezo ya viporo vya mzunguko wa kwanza wa ligi.

Kumbukumbu ya mwisho ya timu hizo kukutana ni ushindi wa mabao 3-2 walioupata Simba Machi 4, 2020 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili msimu uliopita.

Akizungumzia kuhusu maandalizi yao kuelekea mchezo huo, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Kikosi chetu kinaendelea na mazoezi kujiandaa na michezo ya mzunguko wa pili wa ligi, tulianza baada ya kukamilika kwa michuano ya Mapinduzi ambapo tulicheza michezo mitatu ya kujipima nguvu. 

“Kati ya michezo hiyo tulishinda michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja, kabla ya kucheza tena dhidi ya KMC jijini Dar es Salaam.

“Michezo hii ni sehemu ya maagizo ya kocha Lwandamina ambaye kwa kutambua ugumu wa mchezo wetu dhidi ya Simba utakaopigwa Januari 4, ameomba kupatiwa michezo mingi ya kujipima nguvu ili kukifanya kikosi chake kiwe tayari kwa mchezo huo dhidi ya Simba.

“Tunajua Simba wana kikosi kizuri na wameongeza nguvu kupitia usajili lakini hata sisi tumesajili na tumejipanga vizuri,”

 

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic