February 2, 2021



BAADA ya kufunga usajili wao kwa kishindo kwa kumshusha mshambuliaji hatari wa timu ya Taifa ya Burundi, Fiston Abdoul Razak. Uongozi wa klabu ya Yanga umesema hesabu zote zimekamilika na kilichobaki ni vita ya kuhakikisha wanatwaa ubingwa msimu huu.

Fiston aliyetua rasmi siku ya Ijumaa iliyopita akitokea nchini Burundi, na kupelekwa moja kwa moja kujiunga na kambi ya timu hiyo anakamilisha idadi ya wachezaji watatu waliosajiliwa na Yanga katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo.

Wachezaji wengine wa Yanga waliosajiliwa ni; Dickson Job na Saidi Ntibazonkiza, huku Yanga pia ikiongeza nguvu kwenye benchi lake la ufundi kwa kumwajiri kocha msaidizi Nizar Khalfan na kocha wa viungo raia wa Ghana Edem Mortotsi.

Akizungumzia mipango yao katika mzunguko wa pili wa ligi Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM na mjumbe wa kamati ya usajili Injinia, Hersi Said amesema: “Tumekamilisha kwa kiasi kikubwa mipango tuliyokuwa nayo kabla ya kuanza kwa msimu huu, ambapo shabaha yetu kubwa ilikuwa ipo katika maeneo matatu ya utawala bora, idara ya ufundi iliyo thabiti na wachezaji wa kiwango cha juu.

“Kazi hiyo tumeikamilisha kupitia usajili bora wa wachezaji na kuajiri makocha wenye viwango na wakati huu tumebaki na lengo moja tu la kuhakikisha tunaibuka mabingwa msimu huu.


1 COMMENTS:

  1. Ikiwa Simba Super Cup

    NA Yanga Mwananchi Media Day

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic