HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa wachezaji wake wameshaanza mazoezi kwa ajili ya mechi za mzunguko wa pili ambao anaamini kwamba utakuwa na ushindani mkubwa.
Thiery amerithi mikoba ya Zuber Katwila ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Ihefu FC chenye maskani yake Mbeya.
Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, ipo nafasi ya 11 na imecheza jumla ya mechi 18 imekusanya pointi 22 huku vinara wakiwa ni Yanga na pointi zao 44 wakiwaacha kwa jumla ya pointi 22.
Mchezo wao wa mzunguko wa kwanza mbele ya Yanga, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 lilifungwa na Lamine Moro ambaye ni beki mwenye mabao manne na pasi moja ya bao.
Haijawa kwenye ubora wake ndani ya misimu miwili mfululizo na msimu wa 2019/20, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar,Thobias Kifaru aliweka wazi kuwa ulikuwa ni msimu mbaya kwao kutokana na kunusurika kushuka daraja.
Thiery amesema:"Maandalizi yanakwenda vizuri na tunaamini kwamba kila kitu kitakwenda sawa kwa mzunguko wetu wa pili hivyo ni suala la kusubiri muda na kuona kile ambacho vijana watafanya ndani ya uwanja,".
Namungo ilimchimbisha Thiery kwa kile ilichoeleza kuwa mwendo wake haukuwa mzuri ndani ya ligi na kwa sasa timu hiyo inayoshiriki Kombe la Shirikisho ikiwa imetinga hatua ya 32 bora ipo chini ya Kocha Mkuu, Hemed Morroco.
0 COMMENTS:
Post a Comment