YACOUBA Songne, mtambo wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga umesema kuwa uwepo wa nyota mpya, Fiston Abdoul Razack ndani ya kikosi hicho utawaongezea nguvu ya kuendelea kufanya vizuri zaidi.
Ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18 na kufunga mabao 29, Yacouba amehusika kwenye mabao 8.
Amefunga mabao manne na kutengeneza pasi nne ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 ikiwa ni msimu wake wa Kwanza baada ya kujiunga na Yanga inayonolewa na Cedric Kaze akitokea Asante Kotoko.
Fiston amejiunga na Yanga kwa dili la miezi sita akitokea Klabu ya ENPPI ya Misri kwa sasa yupo ndani ya ardhi ya Bongo akiwa ameanza mazoezi na wachezaji wenzake, Kigamboni.
Leo Februari 6 anatarajiwa kuonyesha makeke yake kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya African Sports utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Yacouba amesema:"Ujio wa Fiston utaongeza nguvu ya kupambana ndani ya kikosi hasa ukizingatia kwamba ni mchezaji mzuri na anaweza kufanya kazi ya kufunga na kutengeneza nafasi,".
0 COMMENTS:
Post a Comment