DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kiungo wake mshambuliaji Ibrahim Ajibu ana kazi ya kuongeza juhudi akiwa mazoezini pamoja na uwanjani ili kuwa bora.
Ndani ya Simba ambayo imecheza jumla ya mechi 8 chini ya Gomes baada ya kurithi mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye kwa sasa yupo Morocco, kocha huyo ameongoza kwenye mechi nane.
Katika mechi hizo ni mechi moja Ajibu alianza kikosi cha kwanza ilikuwa ni mbele ya African Lyon ambapo Simba ilishinda mabao 3-0, Uwanja wa Mkapa.
Mabao mawili yalifungwa na Ajibu na bao moja lilifungwa na Perfect Chikwende kwa pasi ya Miraji Athuman.
Kuhusu Ajibu, Gomes amesema:"Ni moja kati ya wachezaji wazuri ila anapaswa kuongeza juhudi zaidi ili awe bora kila wakati na kupata namba kikosi cha kwanza.
"Huwa ninamuona mazoezini anafanya kazi nzuri na ninaamini kwamba akizidi kukazana zaidi atakuwa bora na atafikia malengo ambayo anayo na ya timu kiujumla," .
Macho ya Gomes makali
ReplyDelete