February 28, 2021


 UWANJA wa Stamford Bridge leo Februari 28 majira ya saa 1:30 utachezwa mchezo mkali wa Ligi Kuu England ambao unatarajiwa kuwa mkali mwanzo mwisho.

Ni Thomas Tuchel Kocha Mkuu wa Chelsea ambaye atamkaribisha ndugu yake Ole Gunnar Solskjaer wa Manchester United.

Tambo kwa makocha wote wawili zimetawala ambapo kila mmoja ameweka wazi kwamba anahitaji pointi tatu muhimu.

Kocha wa Chelsea amesema:"Kwenye kila mchezo kwetu tunahitaji ushindi na tuna amini kwamba na washindani wetu wanahitaji ushindi hivyo tutapambana muda wote,".


Kocha wa Manchester United Ole amesema:"Ni ngumu kusema kwamba hatuhitaji ushindi ndani ya uwanja, tutapambana ili kupata matokeo mazuri,".

Tuchel atakosa huduma ya beki mkongwe, Thiago Silva huku United wao nyota wao Paul Pogba, Edinson Cavani hawa ni majeruhi.

 Kwenye msimamo Chelsea ipo nafasi ya tano na pointi zake ni 43 inakutana na United iliyo nafasi ya pili na pointi zake 49.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic