MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi wa Klabu ya Simba, Boniface Lihamwike amesema kuwa moja ya kigezo cha mwanachama kupiga kura ni kuwa amelipa ada ya uanachama.
Leo, Februari 7, Simba itafanya uchaguzi mdogo wa Mwenyekiti wa Wanachama kuziba nafasi ya Sued Mkwabi aliyebwaga manyanga Septemba, 2019.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar na wagombea wawili ni Juma Nkamia na Murtaza Mangungu.
Lihamwike amesema:-“Moja ya kigezo cha kupiga kura ni mwanachama kulipia ada ya uanachama hivyo nje ya ukumbi wa mkutano kutakuwa na eneo maalumu ambalo watatumia wanachama ambao hawajalipa kufanya malipo.
"Wagombea wawili ambao ni Juma Nkamia na Murtaza Mangungu walikidhi vigezo, hawa ndiyo wanawania nafasi hii ambayo iliachwa na Sued Nkwabi,".
Mkutano unatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi na kumalizika mapema ili kutoa nafasi ya mashabiki kuhudhuria mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Azam FC.
Wagombea wote wapo vizuri kukabidhiwa majukumu ya uenyekiti ila suala jengine muhimu kwa simba jumapili ya leo ni mechi ya azam. Hii ni mechi ya kibingwa. Hii ni mechi ya wachezaji kuonesha thamani yao na nazungumzia wachezaji wa simba.Simba ipo vizuri kuliko azam ila azam lazima watabadilika leo.Wataikamia mechi na simba wanapaswa kuwa makini na faulo za kijinga na za hatari kutoka kwa wachezaji wa azam.Mchezaji kama Agrey Morris mara nyingi akizidiwa maarifa huwa na tabia ya kucheza faulo za kijinga sana. Tuliona Frank Dunayo alivyomchezea rafu mbaya shomari kapombe.Kwa timu nyingi ligi kuu Bara njia za kuwafanya simba wasicheze mpira wao ni kuwagonga sidhani kama Azam nao wataingia na staili hiyo.Tatizo la simba hivi karibuni ni umaliziaji. Kwa maana yakwamba katika nafasi sita za wazi za kufunga wanazotengeneza huwa wanafunga moja peke yake.Hii haikubaliki lazima wachezaji waekwe chini kuekwa sawa juu ya suala hilo la matumizi mabaya ya nafasi za kufunga.kama wachezaji wa simba watakuwa wapo sharp leo kunako umaliziaji sioni Azam ikitoka salama leo kwa mkapa.
ReplyDeletematokeo Ndio kama ulivyosikia
ReplyDelete