February 7, 2021


 CHRISTINA Mwagala, Ofisa Habari wa Klabu ya KMC amesema kuwa wachezaji wamekubaliana kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo ndani ya Ligi Kuu Bara. 


Februari 4, KMC iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhìdi ya timu ya Namungo FC, Uwanja wa Uhuru jambo ambalo limewapa nguvu kuendelea pale ambapo wameanzia.


Mchezo huo ulikuwa ni Kiporo kwa Wana Kino Boys ambao falsafa yao ni pira spana,pira mapato, pita kodi. 

Ushindi huo umeifanya KMC iwe nafasi ya sita baadabya kucheza mechi 18 na pointi zake kibindoni ni 25 huku Namungo ikiwa nafasi ya 15 na pointi zake ni 15 baada ya kucheza mechi 15.


Christina amesema:"Ushindi wetu mbele ya Namungo FC ni mwanzo wa kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo kwani kazi bado ni kubwa.


"Tunatambua kwamba mzunguko wa pili utakuwa na ushindani mkubwa hilo lipo wazi nasi pia tutaongeza juhudi ili kupata matokeo chanya ndani ya uwanja,".


Februari 12 itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons,  Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic