Anaandika Saleh Jembe
WAKATI fulani huwa nawasikia baadhi ya viongozi hata mashabiki wakiwatuhumu baadhi ya wachezaji wao kuuza mechi.
Mara nyingi ukitaka uthibitisho huwa hakuna zaidi ya kuelezewa namna wachezaji walivyoacha kukaba na kutoa nafasi kwa wapinzani kufunga bao, kusababisha faulo na kadhalika.
Inawezekana haya mambo yapo kwa kuwa Waswahili wanasema lisemwalo lipo.
Pamoja na hivyo, mimi huamini kumekuwa na mengi sana ya kiufundi ambayo yanawalazimisha baadhi ya viongozi na mashabiki kuamini ni tatizo la kuuza mechi.
Mfano mzuri ni mabao mawili katika mechi ya Simba ikicheza dhidi ya wenyeji wake, Dodoma Jiji pale jijini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Bao la kwanza la Simba, kichwa huru kutoka kwa Kagere akiwa katikati ya mabeki lakini angalia Dodoma Jiji walivyosawazisha kwa kichwa huru katikati ya mabeki wa Simba.
Mabeki hao wa Simba wanaocheza michuano ya kimataifa, walirudia kosa lilelile dakika ya mwisho ya mchezo kuruhusu mchezaji apige kichwa huru na Manula akawa nwokozi wao.
Onyo kwa Simba, kama mabeki wao watakubali kuruhusu makosa yanayofanana na haya katika Ligi ya Mabingwa Afrika, hakika Al Ahly na wengine hawatawaacha na huu ndio uitakuwa mwanzo wa kurudi zile 5 tena.
Katika mechi na Dodoma Jiji, mabeki wa Simba wamefaya kosa hili mara 3. Moja Dodoma wakakosa, 2, likawa bao na 3, Manula kafanya ya ziada lakini Vs Al Ahly, AS Vita au Al Merreikh, INAWEZEKANA ZOTE MABAO.
Safu ya mabeki wa Simba inaongozwa na nyota Joash Onyango pamoja na Pascal Wawa, wengine ni Kened Juma, Ibrahim Ame.
Sio matano tu, Nane
ReplyDeletekila anayefungwa amefanya kosa, anayetoa sare kafanya kosa. Kama sio kufanya makosa yanga asingetoasare 5. WAACHENI SIMBA NA MABEKI WAO. WAKATI SIMBA WANAFUNGWA 5 NA AL AHLY WALIKUWA NA PAUL BUKABA, HAPAKUWA NA KENEDY JUMA WALA ONYANGO. TUSUBIRI TAREHE 12 MAJIBU YATAPATIKANA
DeleteJembe upo sahihi lazima tukubali kukosolewa ni kosa la kizembe mno ambalo lilikua linajirudia mechi na dodoma jiji, naamini mwalim aliliona na atalifanyia kazi, kukosekana kwa onyango kulichangia zaidi kosa lile.
ReplyDeleteHakuna timu isiyofungwa baada ya kufanya makosa. Makundi ni ligi sio mtoano.Hivyo cha maana ni kushinda mechi zako za nyumbani kwanza halafu matokeo mengine baadaye. Timu hiyo inayosakamwa imefungwa goli chache kuliko timu zote kwenye ligi ya nyumbani.Leipzig alifungwa 5 na United kwenye Champions league bado Leipzig wapo kwenye mashindano na United wapi European league.
ReplyDeleteAl Ahly alifungwa 5 ns Mamelodi kwenye CAF Champions league bingwa akawa nani?
Kukosoa ni sawa lakini kudai Simba wasifanye kosa la kufungwa goli la kichwa ni ujinga wa kutotafakari.
Kwani magoli ya kichwa yanahesabika mawili?
Kocha ajizatiti kujua namna ya kucheza ugenini ndio muhimu zaidi.
Sawasawa ndugu, unawaza kama mimi. Suala ni kutimiza malengo. Ukitaka usifungwe kacheze kwenye madimbwi, mpira ninaoujuwa tangu utotoni kufungwa kupo tuu. La msingi pia sisi tunauwezo mkubwa tu wa kufunga lakini mjadala haulekezwe huku hata siku moja.
DeleteManula awe na mawasiliano na mabeki wake awe mkali kidogo. Wawa hayuko vizuri kwenye mipira ya kichwa kwenye mipira ya Kona na krosi.kwa upande mwengine hapa ndipo watanzania tunapofeli kiakili na kuweza kutoboa kirahisi na hapa namzungumzia Kennedy Juma. Kenedi juma licha ya kuwa kasafiri hewani kwa kimo lakini anashindwa kutumia urefu wake Kama silaha ya kukiongezea ubora kipaji chake na kuwa mchezaji anaehitajika zaidi si Simba tu hata Esperence au klabu kubwa yeyote Afica.
ReplyDeleteMechi za Vita na Mazembe za kesho zimeahirishwa ili kuwapa muda zaidi za kujitayarisha na mechi zao za CAF.
ReplyDeleteHapa sisi tumekalia ushabiki wa kijinga wa kushangilia timu za nje zifanikiwe.
Huu ugonjwa unadumaza mpira kwani umeingia hata kwa waandishi kuramani timu fulani isifanikiwe kwani ni timu wasioishabikia.
Timu hizo zikishindwa ndio unaona wanakuja na makala za kushauri na kuponda.
Man United kapigwa goli 6 na Tottenham na Liverpool kafungwa goli 7 na Aston Villa.Southampton kapigwa goli 9 maisha yanaendelea.
Barcelona alitolewa na Bayern aggregate 8 -2.Husikii waandishi wakizungumzia. Ni part of football.
Sijuwi
DeleteKwanini ni sawa Simba kufunga magoli ya kichwa na kona lakini wakifungwa inakuwa maajabu. Simba ni timu ya wanadamu sio robots hivyo wanafanya makosa kama timu zingine.
ReplyDeleteTatizo letu mashabiki huwa hatutaki kukubali kukpsolewa lakini no dhahori kabisa kuwa mabeki walifanya makosa mengi, kuruhusu free header ni udhaifu Sana na ndo maana tulifungqa goli
ReplyDelete