UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya TP Mazembe uliochezwa Februari 2 umewapa nguvu ya kuweza kujua namna gani wataweza kuwakabili wapinzani wao Simba.
Azam FC ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Azam Complex ambapo wapinzani wao Simba walipocheza na TP Mazembe kwenye mchezo wa Simba Super Cup dakika 90 zilikamilika kwa timu hizo kutoshana nguvu bila kufungana.
Azam FC ilianza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Nevere Tigere kwa mpira wa adhabu ambapo lilisawazishwa na nyota wa TP Mazembe Adam Boso akiwa ndani ya 18.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanaamini watapata matokeo chanya mbele ya Simba ndani ya uwanja.
“Kupitia mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe, kocha George Lwandamina kuna kitu amekipata na anaamini kwamba ni kipimo sahihi kwa wachezaji wake kuelekea kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba.
"Taswira kamili kuelekea kwenye mechi zetu za ligi imepatikana na kile ambacho mwalimu alikuwa anahitaji amekipata hivyo hakuna mashaka, sisi tupo tayari kwa ushindani.
"Malengo yetu ni kuona kwamba tunaweza kurejea kwenye ile kasi ambayo tulianza nayo wakati ule wa ligi ikianza hivyo tutapambana kurudi kwenye mstari,".
Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza jumla ya mechi 17 inakutana na Simba iliyo nafasi ya pili na pointi zake ni 38.
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx
UWOYA Avunja UKIMYA Ishu ya H BABA - "NATAMANI KUWA MCHUNGAJI SIKU MOJA"
USISAHU KUWA ILIKUWA MECHI YA KIRAFIKI, MAJIBU YATAPATIKANA KESHO IKIFIKA SAA 12 JIONI
ReplyDeleteHuo uongozi umesema hivyo kweli au umbea wenu tu... Ina maana kila siku mnawauliza kuhusu mechi ya simba? Hamlali mnakesha kuiwangia Simba, hamtaweza. Azam atakufa tu na huo Utopolo wenu pia utapigwa
ReplyDelete