February 5, 2021

 


KUFUATIA kiungo wa Yanga, Carlos Fernandes 'Carlinhos' kuwa nje kwa muda mrefu huku zikienea tetesi kuwa huenda mchezaji akaachwa mwishoni wa msimu huu, hatimaye zimemuibua Mjumbe wa kamati ya usajili wa Yanga na Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said ambaye amefunguka kuwa kiungo huyo bado yupo sana Yanga.

Raia huyo wa Angola alijiunga na Yanga katika usajili wa dirisha kubwa ambapo tangia ajiunge na klabu hiyo amekuwa akipatwa na majeraha ya mara kwa mara.

Akizungumzia kuhusu mkataba wa Carlinhos Injinia Hersi Said amesema kuwa mchezaji huyo wakati anasajiliwa na Yanga alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu, hivyo wanatarajia kumuona akiendelea kucheza ndani ya timu hiyo mpaka mwisho wa mkataba wake na hawana mpango wa kumuacha mchezaji huyo.

“Carlinhos wakati anatua Yanga alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kuitumikia Yanga,hivyo ndiyo kwanza ametumika nusu mwaka, kabakiza mwaka mzima wa kuendelea kucheza na tunatarajia kumuona akiendelea kuichezea Yanga na si kumuacha kama inavyoelezwa.

“Kibaya kwake ni majeraha ambayo amekuwa akiyapata, lakini ni moja kati ya wachezaji wazuri ambao tumejaliwa kuwa nao ndani ya timu yetu, sisi kama viongozi tunaamini kuwa mzunguko wa pili atafanya mambo makubwa na ndio maana bado tunamuamini kuwa atatusaidia,”

 

 

 

10 COMMENTS:

  1. Huyu mchezaji tangu awali sikumwamini, nilimwona hana uwezo wa mikikimiki ya ligi, ni mchezaji wa mabonanza tuu. Na waangola wengi wako vile. Luxury players. Watu wa kazi kwa ukanda huu unawspata DR Congo, Burundi kidogo, Zambia na Zimbabwe kidogo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli nimchezaji wakutumainiwa xn nifund mjanja pia anaujua mpira

      Delete
  2. Kwa hapa bongo hawezi labda tuwauzie barcelona

    ReplyDelete
    Replies
    1. ule mpira wa kupiga pasi hata tufungwe kumi huyu simbilisi ata uweza unadhani? ACHA UTANI HAKUNA TIMU YENYE FALSAFA NGUMU YA MPIRA KAMA WALE KATIKA KLABU ZOTE ULAYA. KATIKA ILE TIMU LAZIMA UWE NA UWEZO MKUBWA WA KUPIGA TOUCH KAMA SIO MSHAMBULIAJI WAKATI, TOFAUTI NA HAPO AISEE UTAPONDWA MPAKA UKOME NA MASHABIKI WAKE. PALE SIO YANGA MCHAZAJI KACHEZA MECHI SIFA BAHARI INA JAA.

      Delete
  3. Tumuache kwanza tuone mzunguko wa pili anafanya nini,kwa upande wangu yuko vizuri.

    ReplyDelete
  4. KISA CARLINHOS SIMBA WAKAAMBIWA WATAKOMA MWAKA HUU, IKAWA ZIIII! SASA HIVI KAJA KIJEBA FISTON TUNASIKIA YALE YALE KILA KUKICHA...ALIENDA TAMBWE YANGA KIMYA KIMYA AKAFUNGA MABAO 26, AMELETWA SARPONG KWA MAKELELE RUNDO HADI LEO GOLI 4 TU. IFIKE MAHALI MASHABIKI WA KITANZANI TUBADILIKE NA TUWE TUNATUNZA KUMBU KUMBU ZA KILA MCHEZAJI ALIYECHEZA HAPA NA MAFANIKIO YAKE. SIO MCHEZAJI HAJAFIKA NCHINI WATU TUNAPANGA FOLENI, TUNA DEKI MPAKA LAMI, AKIFIKA INAKUWA LAANA KAMA. TUMUACHE MCHEZAJI AJE KWA MIGUU YAKE MWENYEWE NA SIO KUANDAMA ANDAMANA, TUACHE MCHEZAJI AJIULIZE HIVI HAWA WATU VIPI MBONA HAWASHTUKI NA MIMI KUJA KATIKA TIMU YAO? KISHA ATAPATA JIBU KUWA YEYE NI KAWAIDA KATIKA HISTORIA YA TIMU, KWA HIYO ANA KAZI YA KUFANYA KUWA NYOTA NA SIO KUPEWA NYOTA NA MASHABIKI WA TIMU

    ReplyDelete
  5. Hii habari ni mara ya pili inaletwa hapa

    ReplyDelete
  6. Tatizo letu wabongo tunashoboka narekodi ya mchezaji aliyo ifanya akiwa natimu zingine huku! Swala nikwamba tumuache acheze kwanza kisha kama uwezo anao ndotumsifie sio tunafanya mapokezi mpaka mchezaji mwenye anabakiakijuiliza hivikweli nitaweza kuendana na dhamna ninayo amina nahawa mashabiki wanao nipokea utazani mimi Rais wa nchi🤣🤣🤣🤣

    ReplyDelete
  7. Yani kachezaji kazuri lakini nafasi anayo cheza sio yako

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic