KAMA ulidhani Simba
Queens watabweteka na likizo ya kusimama kwa Ligi Kuu ya Wanawake, basi utakuwa
umekosea sana kwani kikosi hicho kimemua kufanya mazoezi mara tatu kwa wiki
kabla ya kuanza tena rasmi kambi ya ujumla.
Mpaka Ligi Kuu soka ya
Wanawake inakwenda mapumziko baada ya michezo 11 kupigwa, tayari mabingwa hao
watetezi walikuwa katika nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zao 29.
Akizungumzia mipango waliyonayo kocha mkuu wa kikosi cha Simba Queens, Mussa Mgosi amesema wamefikia maamuzi hayo ili kuhakikisha kikosi chao
kinasalia katika hali ya ushindani ili kufanikisha mpango wao wa kutetea
ubingwa wao.
“Baada ya ligi kusimama
kwa muda kufuatia kukamilika kwa mzunguko wa kwanza, kikosi chetu kiliazimia
kusalia katika hali ya ushindani ambapo tunaendelea na mazoezi tukifanya mara
tatu kwa siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa,”
Kila la kheri
ReplyDelete