February 1, 2021

 




BAADA ya kutua Bongo Januari 29 na kupokelewa na shangwe kutoka kwa mashabiki na viongozi wa Yanga, Fiston Abdulazak Januari 30 alianza mazoezi rasmi na wachezaji wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Nyota huyo ambaye amesaini dili la miezi sita amesema kuwa amekuja kufanya kazi moja ya kufunga mabao jambo ambalo limewafanya Yanga wenyewe wampe jina la mtambo wa mabao.

Habari kutoka kwenye benchi la ufundi ndani ya Yanga linaloongozwa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze raia wa Burundi na mzawa Nizar Khalifan limeeleza kuwa nyota huyo ameanza kuwaka mazoezini huku akipewa jezi namba 7.

“Amekabidhiwa jezi namba 7 ambayo ilikuwa inatumika na Mapinduzi Balama.Balama yeye kwa sasa bado hajatengamaa kwani anaendelea na matibabu.

“Alikuja na kutambulishwa kwa wachezaji na alianza mazoezi tayari na amekuwa akiwashangaza wachezaji wenzake kwa namna alivyo na uwezo katika umiliki wa mpira, na utoaji wa pasi.

“Anaonekana kuwa mwepesi na ana maamuzi ya haraka akiwa na mpira jambo ambalo litakuwa na matokeo mazuri kwetu ligi itakapoanza pamoja na mashindano mengine yatakapoanza hivyo tunasubiri ligi ianze kijana awashe moto,” ilieleza taarifa hiyo.

Spoti Xtra lilimtafuta mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh ambaye alisema kuwa wachezaji tayari wameanza maandalizi kwa ajili ya Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano mengine.

“Kwa sasa wachezaji tayari wameshaanza maandalizi ilikuwa ni tangu Januari 25 tupo kambini. Kwa sasa ni wachezaji watatu ambao wanaendelea vizuri na program zao ambao ni Yacouba Sogne, Saido Ntibanzokiza na Dickson Job kwa kuwa walikuwa ni majeruhi.

“Kuhusu mchezaji Fiston tayari ameanza mazoezi na wenzake,” amesema.

5 COMMENTS:

  1. Kwa maana hiyo Mapinduzi Balama hana chake tena!!!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeambiwa kapewa jezi ya mapinduzi, kwani umeambiwa mapinduzi ndo Basi tena? Jezi zipo nyi nyingi atapewa nyingine

      Delete
  2. Kwa nini apewe jezi yenye mtu, hoyo ina maana mapinduzi ndio kwa heri

    ReplyDelete
  3. Au hana umuhimu kuliko huyu mgeni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic