February 1, 2021


 WEST Ham United walikubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Liverpool, mchezo wa Ligi Kuu England usiku wa kuamkia Januari 31.

Mshambuliaji wa Liverpool, raia wa Misri Mohamed Salah alitupia mabao mawili dakika ya 57 na 68 na lile la tatu lilifungwa na Georginio Wijnaldum dakika ya 84.

West Ham United walipata bao la kufuta machozi kupitia kwa Craig Dawson aliyepachika bao hilo dakika ya 87.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kupanda nafasi moja kutoka ile ya nne mpaka nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 40 ikiwa imecheza jumla ya mechi 21 na West Ham United inabaki nafasi ya tano ikiwa na pointi 35 na imecheza jumla ya mechi 21.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic