February 8, 2021

 


JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa kipa wake Allisson alifanya makosa mawili ambayo yalisababisha timu hiyo ikalala kwa kuchapwa mabao 4-1 mbele ya Manchester City. 

Ikiwa Uwanja wa Anfield, iliruhusu mabao hayo manne na kupoteza pointi tatu muhimu jambo ambalo limewasikitisha Liverpool kwa kuwa walikuwa wanahitaji pointi tatu. 

Mabao ya Manchester City ya Pep Guardiola yalipachikwa na Ikay Gundogan aliyefunga mawili dakika ya 49 na 73, Raheem Sterling dakika ya 76 na Phil Foden dk ya 83.

Mohamed Salah wa Liverpool, alipachika bao kwa penalti dakika ya 63 na kumfanya afikishe jumla mabao 16 akiwa ni kinara wa utupiaji ndani ya Ligi Kuu England. 

Liverpool inabaki nafasi ya nne ikiwa na pointi 40 baada ya kucheza jumla ya mechi 23 huku City ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 50 baada ya kucheza mechi 22.

Klopp amesema:"Wachezaji walicheza vizuri ipo wazi ila ni lazima niseme kwamba Allison alifanya makosa mawili ambayo yalifanya iwe 3-1, labda ni kutojiamini hilo tutalifanyia kazi ili kuona namna gani tutakuwa bora,".

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic