MATHIAS Kigonya, kipa wa timu ya Azam FC amesema kuwa nyota wa Simba, Clatous Chama alipiga penalti ya kawaida jambo ambalo lilimfanya aweze kwenda nayo sawa na kuliweka lango lake salama.
Jana, Februari 7, Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikibwana mbavu na Azam FC, Chama alikosa penalti dakika ya 38 iliyosababishwa na Luis Miquissone ambaye alichezewa faulo ndani ya 18.
Nyota huyo mwenye mabao sita alipiga penalti hiyo iliyookolewa na Kigonya hata aliporejea mara ya pili kupiga wachezaji wa Azam FC waliokoa hatari hiyo jambo lililofanya nyota huyo acheze kinyonge dakika zote 45 za kipindi cha pili.
Kigonya ambaye ni ingizo jipya ndani ya Azam FC kwenye ni nyota wa mchezo huo uliokusanya mabao manne kwa kuwa aliweza kuwakazia washambuliaji wa Simba wakiongozwa na Meddie Kagere mwenye mabao 9.
Kipa huyo amesema:"Ilikuwa ni penalti ya kawaida na jukumu langu mimi ni kuweka lango salama kwa ajili ya timu pamoja na kufikia malengo yangu ambayo nimejiwekea.
"Kupata pointi moja ugenini kwetu sio jambo baya hivyo tutajipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo," .
Sare hiyo inafanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 33 huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi zake ni 39 huku kinara akiwa ni Yanga mwenye pointi 44.
Pia ni mchezo wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kusajiliwa na aliweza kuonyesha uwezo wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment