February 4, 2021

 


KOCHA mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes Da Rosa amefunguka kuwa, ana matumaini makubwa ya kukiongoza kikosi hicho kufika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na ubora wa wachezaji alionao.

Gomes alitambulishwa rasmi na Simba kuchukua mikoba ya aliyekuwa kocha wa kikosi hicho, Sven Vandenbroeck Jumapili ya Januari 24, tayari amekiongoza kikosi hicho katika michezo miwili ya michuano ya Simba Super Cup, akishinda mchezo mmoja na kutoa sare mechi moja.

Leo Alhamisi, Gomes anatarajiwa kuiongoza Simba kwenye mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji.

Akizungumzia uwezo ulioonyeshwa na kikosi chake katika michuano ya Simba Super Cup Gomes amesema: “Kwangu ubingwa tulioupata ni muhimu, lakini jambo la muhimu zaidi ni kuona kikosi changu kikicheza kwa kiwango cha juu katika michezo yetu yote miwili.

“Tuna kikosi chenye hadhi ya kuweza kushindana katika michuano hii mikubwa kwa ngazi ya klabu hapa Afrika, na naamini licha ya mapungufu kidogo ambayo tunapaswa kuyafanyia kazi lakini naamini tutafuzu hatua ya nusu fainali na hata kwenda mbali zaidi ya hapo,”

Simba itaanza kibarua chake kwenye Ligi ya mabingwa Afrika ugenini dhidi ya AS Vita ya DR Congo mchezo utakaopigwa Februari 12 mwaka huu.

7 COMMENTS:

  1. Apambane kwenye suala la mbinu, ufundi, juhudi,stamina na nidhamu

    ReplyDelete
    Replies
    1. APAMBANIE MBINU, NA NIDHAMU NDANI YA UWANJA NA MAZOEZINI, SUALA LA STAMINA MUACHIE ADEL ZRANE

      Delete
  2. Weka rekodi ambayo haitasahaulika na wewe hutosahaulika sio Tanzania tu bali Africa Ya Masharika

    ReplyDelete
  3. UTELEMBWE kama Ute hamvuki makundi, Nguruwe fc nyie

    ReplyDelete
    Replies
    1. Matahira fc A.K.A callendar fc kwenye ubora wenu

      Delete
  4. Dua za kuku Utopolo wahedi. Roho ya uhasidi haiwafikishi kokote.Ohh hamfiki makundi mara paap.
    Unajifanya Meenyezi Mungu wewe Utopolo. Ndio manaa hamuishi kufungiwa kwa kudhulumu wachezsji.Dhulumati wakubwa.

    ReplyDelete
  5. Manyani FC hakukosea Eymael . Timu ipo kwa kuwaangalia wenzao wanafanya nini.Ndio maana wanashindwa lulipa madeni na haki za wachezaji. Unadhulumu haki za wachezaji wavuja jasho utafanikiwa vipi?
    Hawajibiki FIFA sio TFF mtakoma na ujinga wenu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic